Natiq al‑Zarkani alituma ujumbe wa video kwa IQNA kwa mnasaba wa siku arubaini tangu kuuawa shahidi Imam Khamenei, kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika Mapinduzi ya Kiislamu.
Ayatollah Seyyid Ali Khamenei, akiwa pamoja na makamanda na maafisa wa juu wa Iran, aliuliwa shahidi katika shambulio la anga lililohusishwa na Marekani na utawala wa Israeli kwenye ofisi yake jijini Tehran tarehe 28 Februari 2026.
Ujumbe wa al‑Zarkani ulikuwa kama ifuatavyo:
“Damu ya shahidi Ayatullah Seyyid Ali Khamenei imeleta athari chanya katika harakati za mapambano. Tuliingiwa na huzuni na mshtuko mkubwa kutokana na kuuawa kwake shahidi. Lakini kilichotuimarisha sisi na watu wengine wengi ni utukufu na usafi wa damu yake, ambayo imeleta athari nzuri katika mrengo wa upinzani.”
“Athari hii chanya iliunganisha na kuimarisha mshikamano wa taifa la Iran. Damu hii safi iliwakusanya Wairani na kuwafanya wasambaratishe njama za utawala wa Kizayuni na Marekani ambazo zililenga kushawishi taifal la Iran kuinuka dhidi ya serikali yake. Kwa baraka za damu ya kiongozi huyu aliyeuawa shahidi, taifa la Iran lilibaki limeungana na mipango hiyo ikaporomoka.”
“Mwenyezi Mungu ameweka hekima katika jambo hili, ingawa huenda isiwe dhahiri kwa baadhi yetu. Lakini wale wenye ufahamu na busara wanaotazama matukio kwa undani na kuyaona mazuri yaliyomo, wao wanaiona hekima hiyo waziwazi.”
“Ni kweli kwamba tukio hili lilituathiri sana kiroho na kihisia. Ninaamini hakuna muumini wala Mwislamu ambaye hakuguswa na taarifa ya kuuawa shahidi kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei. Lakini kama nilivyosema, kwa neema za Mungu, damu hii safi na isiyo na hatia imeleta manufaa. Tunapokutana na tukio kama hili, tunapaswa pia kutafakari upande wake chanya, hata kama ni wa maumivu na ugumu. Hakika kuna hekima ndani yake ambayo wengine huielewa.”
4345072